• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Baruapepe |
Igunga District Council
Igunga District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Igunga

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Msingi Mkuu
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Halmashauri
    • Idara
      • Maendeleo ya Jamii
      • Afya
      • Idara ya Elimu Msingi
      • Idara ya Elimu Sekondari
      • Utumishi na Utawala
      • Mazingira
      • Maji
      • Ujenzi
      • Kilimo,Umwagiliaji na Ushirika
      • Maliasili, Ardhi na Mazingira
      • Uvuvi na Mifugo
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Fedha na Biashara
    • Vitengo
      • Teknolojia ya Habari na Mawasiliano
      • Uchaguzi
      • Ukaguzi wa ndani
      • Sheria
      • Ugavi
    • Kata
      • Our Wards
  • Vivutio vya Uwekezaji
    • Vivutio Vya Kitalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Uvuvi
  • Wah. Madiwani
    • Orodha Ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha, Uongozi na Utawala
      • Mipangomiji na Mazingira
      • Kamati ya Uchumi, Elimu na Afya
      • UKIMWI
      • Kamati Ya Maadili
    • Ratiba
      • Vikao Vya Madiwani
      • Meeting With Chairperson
  • Miradi
    • Miradi Itakayo Tekelezwa
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Huduma kwa Mteja
    • Mpango Mkatati
    • Ripoti
    • Fomu
    • Taratibu
  • Vituo vya Habari
    • Press Release
    • Video za Shughuli za Ofisi Kitaifa
    • Makitaba ya Picha
    • Hotuba za Viongozi

Farming

Fursa za  kibiashara katika  sekta ya mifugo 

Utangulizi

Sekta ya mifugo ina umuhimu mkubwa katika kujenga uchumi imara ambao utapelekea kuleta usawa baina ya watanzania kwa kuwaongezea kipato na kuwapatia fursa za ajira. Sekta ya mifugo in umuhimu mkubwa maendeleo ya uchumi wa Tanzania kwa kuimarisha usalama wa chakula, kuchangia katika uchumi wa taifa, kuongezeka kwa kipato na kutengeneza fursa za ajira kwa jamii za vijijini na mijini. Mafanikio ya sekta ya mifugo yatatokana na kuwajengea wadau wa sekta ya mifugo kuendesha sekta kisasa na kibiashara kwa kufuga mifugo inayokuwa haraka, yenye uzalishaji mkubwa hivyo kupelekea upatikanaji wa mifugo na mazao ya mifugo bora.

Wilaya ya Igunga ni miongoni mwa Wilaya zenye Mifugo mingi katika Mkoa wa  Tabora ikiwa km za mraba  513 zinafaa kwa malisho ya mifugo na mifugo 1,841,719 kwa mchanganuo ufuatao katika jedwali na.

 Jedwali Na. 1 Takwimu za mifugo wilayani Igunga

Aina ya Mifugo

Idadi

Asili

Kisasa

Ng’ombe

685,416

1,876

Mbuzi

364,252

178

Kondoo

195,024

0

Kuku

552,615

                                             4081

Bata

5,181

0

Nguruwe

9,200

17

Punda

11,055

0

Mbwa

9,182

0

Paka

3,642

0

Jumla

1,835,567

6,152

 

Fursa katika sekta ya mifugo

Zipo fursa nyingi zinazoweza kuongeza mchango wa mifugo katika uchumi na uhakika wa chakula kuanzia ngazi ya kaya,Halmashauri na Taifa ikiwa fursa hizo zitatumika ipasavyo,fursa hizo ni pamoja na:.

  • Idadi kubwa ya mifugo ya aina mbalimbali ikiwemo ,ng’ombe,mbuzi,kondoo, punda ,kuku na  nguruwe (angalia jedwali hapo juu)

Idadi kubwa ya mifugo hii ni ya asili, hata hivyo pamekuwa na ongezeko kubwa la idadi ya ng’ombe wa maziwa kutoka ng’ombe 70 mwaka 2005 hadi ng’ombe  1876  mwaka 2017, pia  uzito wa ng’ombe kutoka  kilo 200 mwaka 2005 hadi kilo 500 mwaka 2017.

Ndama bora aliyetokana na upandishaji kwa kutumia dume bora.

  • Eneo kubwa la ardhi llinalofaa kwa malisho Ha 513,000  ambalo linaweza kuboresheshwa kwa kuweka miundombinu ya nyanda za malisho (k.m malambo, majosho,vibanio) na uboreshaji wa malisho kwa kupandikiza mimea ya malisho bora.

Masoko ya uhakika ya mifugo na mazao yake,mji wa Igunga upo katika barabara kuu ya Dar-es Salaam,Mwanza,Tabora,Kahama,Kigali,Bunjumbura,Goma na Kampala,hii ni fursa muhimu kwa mifugo na mazao yake. Mji wa Igunga una huduma zote muhimu za kijamii ( afya,usafiri,malazi,mahoteli safi, umeme) na kifedha (NMB CRDB, ,Mpesa ,Tigo Pesa na Airtel Money, Halopesa)

Upatikanaji wa watu wanaoweza kufunzwa na gharama nafuu za nguvu kazi.

Halmashauri ina wataalam katika sekta mbalimbali k.v mifugo,kilimo,ardhi,mazingira, maendeleo ya jamii,ushirika utawala, maji na fedha wanaounda timu kabambe ya wawezeshaji wa wilaya.

Halmashauri imetenga ekari 157.69 kwa ajili ya viwanda vidogo na ekari 84 kwa ajili ya viwanda vikubwa, maeneo haya yanaweza kutumika kwa ajili ya viwanda vya ngozi, maziwa ,nyama na vyakula vya mifugo.

Vivutio vya uwekezaji katika sekta ya mifugo

  • Eneo la nyanda za malisho linaloweza kutumika kuanzisha mashamba ya kuzalisha mbegu bora za malisho kwa ajili ya uboreshaji wa malisho ya asili na hivyo kuongeza ubora na wingi wa lishe ya mifugo.
  • Barabara kuu inayounganisha wilaya, mikoa na nchi jirani za Jamhuri ya Kidemokrasia Kongo, Rwanda, Burundi, Uganda na Kenya.
  • Wilaya ina eneo la nyanda za malisho linaloweza kutumika kuanzisha mashamba ya kuzalisha mitamba au vituo vya kunenepesha ng’ombe wa nyama na kuwauza katika viwanda vya nyama. (Bulyashiri Ha 320 na Uswaya Ha 300)
  • Wilaya ya Igunga ina idadi kubwa ya mifugo ya asili ambayo ikiboreshwa ina uwezo mkubwa katika uzalishaji.
  • Halmashauri ina eneo maalumu kwa ajili ya kiwanda cha nyama na mazao yake.
  • Kituo cha Uchunguzi wa magonjwa ya mifugo cha Kanda ya Magharibi (VIC) kipo mkoani Tabora ambapo ni fursa kubwa katika kubaini na kutokomeza magonjwa mbalimbali ya mifugo yanayoathiri ukuaji wa sekta.
  • Wataalam wa mifugo katika fani mbalimbali za sekta ya mifugo ( Tiba, uzalishaji, malisho na ugani).
  • Vikundi  85 vya uzalishaji wa mifugo vinavyoweza kuingia ubia na wawekezaji
  • Sera nzuri  na endelevu za mifugo na uchumi
  • Taasisi binafsi zinazoshirikiana na Halmashari katika kutoa huduma na kuendeleza sekta ya mifugo, taasisi hizo ni pamoja na World Vision,Heifer Project International,Kanisa Katoliki,Jida n.k
  • Miundombinu ya mifugo kama vile minada 3, majosho 20,machinjio 1, mawe ya kuchinjia 6, vituo vya afya ya mifugo 7
  • Mji wa Igunga una huduma zote muhimu za kijamii ( barabara, afya,usafiri,malazi,mahoteli safi, umeme) na kifedha (NMB,Mpesa ,Tigo Pesa na Airtel Money)
  • Mradi mkubwa wa maji kutoka ziwa Viktoria utawezesha upatikanaji wa maji ya uhakika kwa ajili ya viwanda na matumizi mengine.
  • Mradi wa bomba la mafuta kutoka Uganda utaongeza idadi ya watu na mahitaji.
  • Uwepo wa Amani na usalama katika Wilaya.

Uwekezaji unaweza kufanyika katika maeneo yafuatayo:-

Kuanzisha vituo vya kunenepesha ng’ombe (Mnada wa Igunga, Mnada wa Iborogero na Shamba la Bulyashiri).

Viwanda vya usindikaji wa nyama ( kuchinja kwa ajili kupeleka kwenye viwanda vikubwa).

Viwanda vya usindikaji wa maziwa ( kituo cha  kukusanya na kupooza maziwa kwa ajili ya viwanda).

Viwanda vya usindikaji wa ngozi

Kuanzisha vituo vya kukusanya,kukagua, kuchinja na kuuza kuku

uzalishaji wa vyakula vya mifugo

Uwekezaji kwenye masoko ya mifugo (mabucha,majiko,meza n.k)

 

Takwimu za ongezeko la miundombinu na uzalishaji wa mifugo

 
Sekta ya mifugo
2014/2015
2017/2018
Asilimia ya ongezeko
1
Banda la ngozi
1
2
50
2
Ng’ombe bora wa maziwa
1123
1876
67
3
Majosho
19
20
5
4
Madume bora ya ng’ombe
262
603
130
5
Mashamba darasa
3
7
133
6
Vikundi vya wafugaji
21
62
195
8
Minada ya mifugo
3
4
33
9
Uzalishaji wa mazao ya mifugo
Nyama (tani)
449.68

642.4

30
Maziwa (lita)
61,687,427

65,774,080

6.6
Mayai
 4,752,798

6,789,712

30

Matukio ya magonjwa yanayoenezwa na kupe (Ndigana kali na baridi,kukojoa damu na majimoyo) yamepungua kutoka asilimia 70%  mwaka 2010 hadi asilimia 30%.mwaka 2017.

Uzito wa ng’ombe wa miaka 3-5 kutoka kilo 150-200 hadi kilo 350-500 kwa ng’ombe

 


Matangazo

  • TANGAZO LA KUKODISHA SHAMBA LA BULYASHIRI LINALOMILIKIWA NA H/W IGUNGA October 03, 2022
  • TANGAZO LA KUITWA KAZINI IGUNGA DC September 05, 2022
  • TANGAZO LA NAFASI YA KAZI MAALUMU YA KUKUSANYA USHURU HALMASHAURI YA WILAYA YA IGUNGA August 24, 2021
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI November 24, 2020
  • View All

Habari Mpya

  • JOGGING PAMOJA NA MAZOEZI

    March 05, 2023
  • BARAZA LA MADIWANI LAPITISHA BAJETI YA MWAKA 2023/2024

    March 05, 2023
  • Mh.Mkuu wa Wilaya Igunga Akabidhi Pikipiki Saba kwa Watendaji wa Kata Wilayani Igunga

    March 01, 2023
  • ZIARA YA KATIBU UENEZI CCM TAIFA WILAYA YA IGUNGA

    September 13, 2022
  • View All

Video

Maadhimisho ya siku Wanawake Kata Simbo ya SIMBO wilayani Igunga.
Video Zaidi

Viungio vya haraka

  • Hotuba
  • Pakua Fomu
  • Zabuni
  • Matangazo ya kibiashara
  • Matukio

Kurasa zinazofanana

  • Watumishi Portal
  • Poralg
  • Public Service Management
  • Tabora Region Website
  • NECTA

World visitors tracker

world map hits counter

Waliotembelea

writingMasterThesis

Ramani

Wasiliana nasi

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya mara kwa mara
    • Sitemap
    • Huduma
    • Huduma

Hatimiliki@2017Halmashauri ya Wilaya ya Igunga. Haki zote zimehifadhiwa