• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Baruapepe |
Igunga District Council
Igunga District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Igunga

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Msingi Mkuu
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Halmashauri
    • Idara
      • Maendeleo ya Jamii
      • Afya
      • Idara ya Elimu Msingi
      • Idara ya Elimu Sekondari
      • Utumishi na Utawala
      • Mazingira
      • Maji
      • Ujenzi
      • Kilimo,Umwagiliaji na Ushirika
      • Maliasili, Ardhi na Mazingira
      • Uvuvi na Mifugo
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Fedha na Biashara
    • Vitengo
      • Teknolojia ya Habari na Mawasiliano
      • Uchaguzi
      • Ukaguzi wa ndani
      • Sheria
      • Ugavi
    • Kata
      • Our Wards
  • Vivutio vya Uwekezaji
    • Vivutio Vya Kitalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Uvuvi
  • Wah. Madiwani
    • Orodha Ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha, Uongozi na Utawala
      • Mipangomiji na Mazingira
      • Kamati ya Uchumi, Elimu na Afya
      • UKIMWI
      • Kamati Ya Maadili
    • Ratiba
      • Vikao Vya Madiwani
      • Meeting With Chairperson
  • Miradi
    • Miradi Itakayo Tekelezwa
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Huduma kwa Mteja
    • Mpango Mkatati
    • Ripoti
    • Fomu
    • Taratibu
  • Vituo vya Habari
    • Press Release
    • Video za Shughuli za Ofisi Kitaifa
    • Makitaba ya Picha
    • Hotuba za Viongozi

Wilaya ya Igunga yazindua rasmi Timu ya Ulinzi na Usalama wa Mtoto

Tarehe iliyowekwa: June 9th, 2017

Kwa ufadhili wa shirika la World Vision limezindua timu hiyo ya Ulinzi na Usalama wa Mtoto katika Halmashauri ya Wilaya ya Igunga ambayo itakuwa na jukumu la kuhakikisha kuwa Haki za mtoto zinazingatiwa na kutekelezwa kwa mujibu wa Sheria.

Uzinduzi huo ulifanywa na Mkuu wa Wilaya ya Igunga aliyewakirishwa na Katibu Tarafa Igunga ndugu Shadrack Pastory Kalekayo, iliyofanyika katika ukumbi wa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Igunga tarehe 05 Juni, 2017 na kuhudhuriwa na viongozi mbali mbali ambao ni wadau wa watoto wakiwemo Wataalam wa Halmashauri (kutoka Idara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Elimu, Mipango),  wajumbe wa kamati ya Ulinzi na Usalama  ya Wilaya ( Mkuu wa gereza la Igunga, Mshauri wa Mgambo, Afisa Uhamiaji na Dawati la jinsia Polisi), mwakilishi wa NGOs, Wawakilishi wa madhehebu ya Dini na mwakilishi wa Walimu.

.Akizungumzia kuundwa kwa timu ya ulinzi na usalama wa mtoto, Shadrack kalekayo, alisema kutakuwa na faida kubwa baada ya kuanza kutekelezwa kwa mpango huo kwa ushirikiano wa Halmashauri na ufadhili wa Shirika la World Vision.

Aliongeza kuwa faida ya kuundwa kwa timu hii ni itasaidia kupunguza vitendo vya ukatili wanaofanyiwa watoto katika maeneo mbalimbali ikiwemo majumbani, migodini, mashamba ya kilimo cha umwagiliaji n.k, baadhi ya ukatili wanaokutana nao watoto ni pamoja na ukatili wa kihisia ambapo mtoto anakutana na matusi, kinyimwa chakula, kuto thaminiwa, ukatili wa kimwili inaambatana na vipigo,kukatwa viungo vya mwili, kuchomwa moto, kutumikishwa, ukatili wa kingono inahusisha kubakwa, kulawitiwa, na ndoa za utotoni.

Shadrack aliendelea kwa kusisitiza kwamba timu ikasaidie kuelezea Suala la ulinzi wa mtoto kuwa ni jukumu la jamii nzima, mlezi na mzazi mmoja mmoja kwa nafasi yake katika ngazi ya familia pamoja na serikali kwa ujumla. Ushirikiano katika malezi ya mtoto kati ya wazazi, walezi pamoja na jamii unahitajika kwa kiwango kikubwa ili kuhakikisha usalama wa mtoto. Sehemu nyingine ya muhimu ni ushirikiano na mahusiano ya karibu kati ya mwalimu na mzazi ili kuhakikisha miendendo ya mtoto darasani, mtaani hadi nyumbani.

Akahitimisha kwa kusema, Ieleweke kwamba mzazi, jamii na serikali tukishirikiana hatuwezi hata siku moja kuwaona watoto wakiwa mitaani wanazurura muda ambao wanatakiwa kuwa kwa wazazi wao au shuleni nasi tukabaki kimya. Tuhoji pale tunapowaona madukani wakinunua vilevi, sigara, n.k. Vinginevyo tutarajie ongezeko la watoto wanaoishi na kufanya kazi mitaani, watoto wanaotumia madawa ya kulevya, watoto wanaojihusisha na biashara ya haramu ya ngono, n.k.

Matangazo

  • MATOKEO YA USAILI WA KUANDIKA MSAIDIZI WA KUMBUKUMBU DARAJA II October 12, 2024
  • MATOKEO YA USAILI WA KUANDIKA MTENDAJI WA KIJIJI DARAJA LA III October 12, 2024
  • TANGAZO LA KUITWA KAZINI WATENDAJI WA VIJIJI DARAJA III October 15, 2024
  • TANGAZO LA KAZI July 16, 2024
  • View All

Habari Mpya

  • MHE. DC. SAUDA MTONDOO AWATAKA MADIWANI KUTEMBEA KIFUA MBELE UTEKELEZAJI ILANI YA CHAMA CHA MAPINDUZI IGUNGA

    May 16, 2025
  • MHE. DC. SAUNDA MTONDOO APIGA MARUFUKU KUWEKA MAJI, MAWE NA MCHANGA LAINI KWENYE PAMBA

    May 16, 2025
  • DED IGUNGA AWATAKA WENYEVITI WA VIJIJI NA VITONGOJI KUDUMISHA UADILIFU BUSARA NA HEKIMA KUWAHUDUMIA WANANCHI

    May 10, 2025
  • MHE. RC. PAUL MATIKO CHACHA NA MHE. DC. SAUDA MTONDOO WAICHANGAIA IGUNGA UNITED SH. MILIONI 1.8

    April 22, 2025
  • View All

Video

Maadhimisho ya siku Wanawake Kata Simbo ya SIMBO wilayani Igunga.
Video Zaidi

Viungio vya haraka

  • Hotuba
  • Pakua Fomu
  • Zabuni
  • Matangazo ya kibiashara
  • Matukio

Kurasa zinazofanana

  • Watumishi Portal
  • Poralg
  • Public Service Management
  • Tabora Region Website
  • NECTA

World visitors tracker

world map hits counter

Waliotembelea

writingMasterThesis

Ramani

Wasiliana nasi

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya mara kwa mara
    • Sitemap
    • Huduma
    • Huduma

Hatimiliki@2017Halmashauri ya Wilaya ya Igunga. Haki zote zimehifadhiwa