• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Baruapepe |
Igunga District Council
Igunga District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Igunga

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Msingi Mkuu
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Halmashauri
    • Idara
      • Maendeleo ya Jamii
      • Afya
      • Idara ya Elimu Msingi
      • Idara ya Elimu Sekondari
      • Utumishi na Utawala
      • Mazingira
      • Maji
      • Ujenzi
      • Kilimo,Umwagiliaji na Ushirika
      • Maliasili, Ardhi na Mazingira
      • Uvuvi na Mifugo
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Fedha na Biashara
    • Vitengo
      • Teknolojia ya Habari na Mawasiliano
      • Uchaguzi
      • Ukaguzi wa ndani
      • Sheria
      • Ugavi
    • Kata
      • Our Wards
  • Vivutio vya Uwekezaji
    • Vivutio Vya Kitalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Uvuvi
  • Wah. Madiwani
    • Orodha Ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha, Uongozi na Utawala
      • Mipangomiji na Mazingira
      • Kamati ya Uchumi, Elimu na Afya
      • UKIMWI
      • Kamati Ya Maadili
    • Ratiba
      • Vikao Vya Madiwani
      • Meeting With Chairperson
  • Miradi
    • Miradi Itakayo Tekelezwa
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Huduma kwa Mteja
    • Mpango Mkatati
    • Ripoti
    • Fomu
    • Taratibu
  • Vituo vya Habari
    • Press Release
    • Video za Shughuli za Ofisi Kitaifa
    • Makitaba ya Picha
    • Hotuba za Viongozi

WANANCHI WATAKIWA KUPIMA UKIMWI KUJUA AFYA ZAO WAWALINDE WENZAO NA KUBAKI NJIA KUU

Tarehe iliyowekwa: December 2nd, 2024

MKURUGENZI Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Igunga mkaoni Tabora, Bi Selwa Abdalla Hamid amewakumbusha wananchi umuhimu wa kutunza afya zao na kutakiwa kuwa na tabia za kutembelea Hospitali kwa sababu watagundua umuhimu wa hilo.

Bi, Selwa ameyasema hayo Jumapili Desemba 01, 2024 katika Maadhimisho ya Siku ya UKIMWI duniani yaliyofanyika katika Kata ya Ibologero kijiji cha Ibologero mjini hapa.

“Ndugu wananchi niwasihi tuendelee kujilinda sisi na ndugu au familia zetu dhidi ya gonjwa la UKIMWI,’’ amesema.

Katika hatua nyingine, Bi. selwa amewataka watu waliokwisha ambukizwa gonjwa hilo kutokua na tabia ya kuwaambukiza wengine kwa sababu kufanya hivyo ni sawa na  kuangamiza Taifa na kutenda dhambi kwa kumuhujumu mtu kwa makusudi.

Amesema ni vyema kila mmoja akawa na tabia ya kwenda kupima kwa lengo la kuelewa hali yake ya maambukizi ikoje aidha ameambukizwa au la na wasiogope kufanya hivyo kwa kuwa upo usiri wa kutunza taarifa zao.

Ameweka wazi kuwa katika wilaya hii kunawananchi takribani 546,204 ambapo katika hao watu 938 wamekwisha ambukizwa huku asilimia 71 wanajitambua na asilimia 29 hawajitambui jambo ambalo ni hatari.

Amesema njia sahihi ina maana pana ikiwemo wale waliofika umri waendelee kubakika katika ndoa zao huku akiwakumbusha tabia ya kuwa na mchepuko sio njia sahihi.

Aidha, amewahamasisha wananchi kuwa na tabia ya kupanda miti nakuacha  kukata miti huku akiahidi kutoa miti kwa watu ambao watakua wamejipanga kupanda miti.

“Nitoe wito ndugu zangu katika maeneo yenu mpande miti na watakao kosa miche mimi nitawasaidia kwa lengo la kuhakikisha Igunga yetu inabaki kuwa ya kijani na kuwaachia vizazi vijavyo mazingira salama,” amessistiza.

Akizungumza katika Hafla hiyo Afisa Tarafa ya Manonga ambae ni Mwakilishi wa Mkuu wa Wilaya hiyo, Martha Tevel amewashukuru Wadau wa Maendeleo ambao wamekuwa wakishirikiana na Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Mhe. Rais Dk. Samia Suluhu Hassan kutokomeza janga la UKIMWI.

Awali akiwasilisha taarifa ya hali halisi ya maambukizi ya UKIMWI  Mratibu wa UKIMWI ngazi ya jamii wa wilaya hiyo, Devotha Macheku amefafanua maana ya kauli mbiu ya maadhimisho hayo isemayo  “Chagua Njia Sahihi Tokomeza UKIMWI” kuwa ni mtu akipima na kugundulika kuwa amepata maambukizi ya Virusi vya UKIMWI ajiunge na huduma ya matunzo na tiba.








Matangazo

  • MATOKEO YA USAILI WA KUANDIKA MSAIDIZI WA KUMBUKUMBU DARAJA II October 12, 2024
  • MATOKEO YA USAILI WA KUANDIKA MTENDAJI WA KIJIJI DARAJA LA III October 12, 2024
  • TANGAZO LA KUITWA KAZINI WATENDAJI WA VIJIJI DARAJA III October 15, 2024
  • TANGAZO LA KAZI July 16, 2024
  • View All

Habari Mpya

  • MHE. DC. SAUDA MTONDOO AWATAKA MADIWANI KUTEMBEA KIFUA MBELE UTEKELEZAJI ILANI YA CHAMA CHA MAPINDUZI IGUNGA

    May 16, 2025
  • MHE. DC. SAUNDA MTONDOO APIGA MARUFUKU KUWEKA MAJI, MAWE NA MCHANGA LAINI KWENYE PAMBA

    May 16, 2025
  • DED IGUNGA AWATAKA WENYEVITI WA VIJIJI NA VITONGOJI KUDUMISHA UADILIFU BUSARA NA HEKIMA KUWAHUDUMIA WANANCHI

    May 10, 2025
  • MHE. RC. PAUL MATIKO CHACHA NA MHE. DC. SAUDA MTONDOO WAICHANGAIA IGUNGA UNITED SH. MILIONI 1.8

    April 22, 2025
  • View All

Video

Maadhimisho ya siku Wanawake Kata Simbo ya SIMBO wilayani Igunga.
Video Zaidi

Viungio vya haraka

  • Hotuba
  • Pakua Fomu
  • Zabuni
  • Matangazo ya kibiashara
  • Matukio

Kurasa zinazofanana

  • Watumishi Portal
  • Poralg
  • Public Service Management
  • Tabora Region Website
  • NECTA

World visitors tracker

world map hits counter

Waliotembelea

writingMasterThesis

Ramani

Wasiliana nasi

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya mara kwa mara
    • Sitemap
    • Huduma
    • Huduma

Hatimiliki@2017Halmashauri ya Wilaya ya Igunga. Haki zote zimehifadhiwa