Afisa Elimu Msingi Wilaya ya Igunga Bibi Dora Stephen Simbachawene, amewataka walimu wa hisabati wa darasa la kwanza na la pili, kufata maelekezo waliyopewa na wakufunzi na yaliyopo kwenye moduli ya mwalimu ya 10 hadi 13, akifungua mafunzo kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji Wilaya ya Igunga kwa walimu wa hisabati katika shule ya msingi chipukizi na igunga zilizopo mjini Igunga hivi karibuni.
Bibi Dora amesema mafunzo haya yatasaidia kuwapa umahiri walimu wa hisabati wa darasa la kwanza na darasa la pili wa shule za Serikali 133, pamoja na walimu waratibu wa mafunzo 133 kutoka shule zote za Serikali, ambao wamefikia jumla ya 226 katika mafunzo haya.
“Mafunzo yatasaidia wanafunzi kujua kusoma, kuandika na kuhesabu KKK, ili kufanikisha kufuta madarasa ya KKK katika halmashauri ya Wilaya ya Igunga” alisema Bibi Dora Stephen Simbachawene, Afisa Elimu msingi Wilaya ya Igunga.
“Mafunzo haya ni mwendelezo wa moduli ya kwanza hadi ya tisa ambazo zilishafundishwa na kumwezesha mwalimu kufundisha, mafunzo hayo yanakamilisha mahiri hizo za kuandika, kusoma na kuhesabu” aliongeza Bibi Martha Bayo Mratibu wa Mradi wa EQUIP-Tanzania Wilaya ya Igunga.
“Walimu wamefundishwa mbinu za kufundisha kuhesabu ambapo ndani yake kuna kuandika, kusoma na kuhesabu KKK , mratibu wa mafunzo ataandaa mafunzo kwa walimu wote ili kuwajengea uwezo wa kufundisha mahiri hizo bila kuangalia mwalimu huyo ni wa darasa la saba”aliongeza bwana Edger Kulwa, Afisa Elimu taaluma Wilaya ya Igunga.
Katika kuongenza ufanisi wa ufundishaji na ujifunzaji, taasisi ya Elimu Tanzania kwa kushirikiana na EQUIP-Tanzania, wameandaa moduli ambazo zimesheheni mbinu mbalimbali za ufanisi za ufundishaji na ujifunzaji.
Mwalimu Henry Munkizi shule ya Msingi Bugayambelele Kata ya Choma, amekiri kuwa mafunzo yamewezesha kunijengea uwezo wa kuwa mahiri katika kufundisha soma la hisabati na nitajitahidi kuwa chachu ya kufikisha mbinu mpya za kufundisha somo la hisabati kwa darasa la I na darasa la II.
Naye Mwalimu Mariam Stuwat Mratibu wa mafunzo shule ya Msingi Iborogelo kata ya Iborogelo, amekubali kuwa mafunzo haya yamekuwa chanchu kwa walimu na waratibu wa mafunzo katika Wilaya ya Igunga na yatawezesha kuongeza ufanisi wa ufundishaji na ujifunzaji kwa somo la hisabati darasa la I na darasa la pili.
Vile vile moduli inatoa mafunzo ya ziada ikitarajiwa kuwa walimu watakuwa wamekwishapata mafunzo kabilishi ya utekelezaji wa mtaala ulioboreshwa wa kuimarisha ufundishaji kusoma, kuandika na kuhesabu KKK kwa wanafunzi wa darasa la I na darasa la pili katika Wilaya ya Igunga.
Hatimiliki@2017Halmashauri ya Wilaya ya Igunga. Haki zote zimehifadhiwa