BAADHI ya Viongozi kutoka Wizara ya Katiba na Sheria wametoa mafunzo ya uraia na utawala bora kwa viongozi mbalimbali wa Halmashauri ya wilaya ya Igunga mkoani Tabora.
Viongozi hao wametoa mafunzo hayo Jumatatu Februari 03, 2025 katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri hiyo mjini hapa.
Aidha, viongozi hao waliwakumbusha washiriki wa mafunzo hayo kuhusu Madaraka kwa umma, Demokrasia na Utawala Bora, Ulinzi na Usalama wa Inchi na haki na wajibu.
==== //// ==== //// ====
Hatimiliki@2017Halmashauri ya Wilaya ya Igunga. Haki zote zimehifadhiwa