Halmashauri ya Wilaya ya Igunga inaendelea kufanya kazi ya kuleta maendeleo katika sekta mbalimbali za kiuchumi na kijamii kwa kushirikiana na wadau wa maendeleo wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali (NGOs).
Halmashauri ya Wilaya ya Igunga kupitia Idara ya Maendeleo ya Jamii imeendelea kutekeleza shughuli mbalimbali za maendeleo kwa jamii kwa kushirikiana na wadau wa Mashirika yasiyo ya kiserikali ambao wanaratibiwa chini ya dawati maalum la Uratibu wa Mashirika yasiyo ya kiserikali (NGOs) lililopo Idara ya Maendeleo ya Jamii lililoanzishwa kupitia “Mwongozo wa Majukumu ya Maafisa Maendeleo ya Jamii” mwaka 2019.
Usimamizi wa shughuli za Mashirika Yasiyo ya Kiserikali (NGOs) unatekelezwa chini ya “Sera ya Taifa ya Mashirika Yasiyo ya Kiserikali ya mwaka 2001 ikiwa na Sheria ya Mashirika Yasiyo ya Kiserikali Na. 24 ya mwaka 2002 kama ilivyofanyiwa marekebisho na Sheria Na. 11 ya mwaka 2005 na Sheria Na. 3 ya mwaka 2019 na kufuatiwa na Mwongozo wa Uratibu wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali Tanzania Bara wa mwaka 2020’’.
MASHIRIKA YANAYOTEKELEZA MIRADI YAKE KATIKA WILAYA YA IGUNGA
Halmashauri ya Wilaya ya Igunga ina wadau wapatao 11 ambao wanatekeleza miradi yao katika sekta mbalimbali za Maendeleo hapa wilayani.
Katika idadi hiyo Mashirika sita (6) yanaendelea na utekelezaji wa miradi yao, Mashirika matatu (3) yamemaliza muda wa utekelezaji wa miradi yao na Mashirika mawili (2) wamepokelewa na kutarajia kuanza miradi yao mwezi Oktoba, 2023.
Mashirika Yasiyo ya Kiserikali (NGOs) yanayotekeleza miradi yake hapa wilayani yamekuwa na mchango chanya katika kuchochea maendeleo kwa jamii zetu kwa kuleta/kusogeza huduma mbalimbali za kijamii na kiuchumi zinazosaidia kupunguza adha na changamoto zinazozunguka jamii hizo.
SHUGHULI ZILIZOTEKELEZWA KATIKA ROBO YA JULAI-SEPTEMBA, 2023.
Mhe. Mwenyekiti, Katika kipindi cha robo ya kwanza ya Julai-Septemba ya mwaka wa fedha wa 2023 / 2024 Halmashauri imetekeleza yafuatayo:-
MAFANIKIO
katika usimamizi wake Halmashauri imeweza kufanikiwa yafuatayo:-
ORODHA YA MASHIRIKA YANAYOTEKELEZA MIRADI YAKE WILAYANI IGUNGA
1. MASHIRIKA YASIYO YA KISERIKALI WANAOENDELEA NA UTEKELEZAJI WA MIRADI |
||||||
NA. |
JINA LA SHIRIKA
|
MRADI UNAOTEKELEZA
|
JUMLA YA THAMANI YA MRADI |
SEKTA |
MFADHILI
|
WANUFAIKA
|
1 |
Igunga Paralegal Center (IPC)
|
Upatikanaji wa Haki Kwa Jamii
|
12,500,000.00 |
Sheria |
Legal Service Facility - Tanzania
|
Makundi Maalum
|
2 |
Management and Development of Health (MDH)
|
Afya Jumuishi
|
1,243,000,000 |
Afya |
CDC / PEPFAR
|
Makundi hatarishi (AYGW) na Makundi Waathirika (PLHIV)
|
3 |
Inland Development Tanzania (IDT)
|
ACHIEVE
|
105,592,800.00 |
Afya |
United States Agency for International Development (USAID)
|
Watoto wanaoishi na maambukizi ya VVU/UKIMWI umri wa miaka 0-17
|
4 |
Johns Hopkins Program for International Education in Gynecology and Obstetrics (JHPIEGO)
|
TOHARA
|
|
Afya |
United States Agency for International Development (USAID)
|
|
USAID AFYA YANGU
|
|
Afya |
United States Agency for International Development (USAID)
|
Wajawazito na watoto wachanga , Afya ya Watoto, Lishe, Chanjo, Vijana 10-24.
|
||
5 |
Elizabeth Glasser Pediatric Aids Foundation (EGPAF)
|
USAID AFYA YANGU-NORTHERN ZONE
|
78,452,656.00 |
Afya |
United States Agency for International Development (USAID)
|
Wagonjwa wa Kifua Kikuu
|
MALEZI NA MAKUZI
|
12,000,000.00 |
Ustawi wa Jamii |
Conrad Hillton Foundation
|
Watoto chini ya miaka 5
|
||
6 |
Compassion (Vituo 4 vya Makanisa)
|
Huduma ya mtoto na Kijana
|
37,200,000.00 |
Jamii |
Compassion Tanzania
|
Watoto na Vijana
|
2. MASHIRIKA YALIYOMALIZA UTEKELEZAJI WA MIRADI YAKE |
||||||
7 |
Media for Development and Advocacy (MEDEA)
|
SAUTI ZETU
|
182,000,000.00
|
Jamii |
MALALA FUND
|
Mabinti
|
8 |
National Council of People Living with HIV (NACOPHA)
|
HEBU TUYAJENGE PROJECT
|
20,145,000.00 (kwa mwaka) |
Jamii |
United States Agency for International Development –(USAID)
|
Wanaoishi na Virusi vya UKIMWI
|
9 |
Jikomboe Integral Development Association (JIDA)
|
USAID AFYA YANGU
|
144,000,000.00 |
Jamii |
USAID - JHPIEGO
|
Watoto waishio mazingira hatarishi
|
3. MASHIRIKA YALIYOHAKIKIWA KUANZA UTEKELEZAJI MWEZI OKTOBA, 2023. |
||||||
10 |
Thubutu Africa Initiative (TAI)
|
USAID AFYA YANGU
|
|
Jamii |
USAID - JHPIEGO |
Wanawake , Watoto na Vijana 10-24.
|
11 |
BRAC Maendeleo
|
UWEZESHAJI WA WASICHAN A NA WANAWAKE KIJAMII NA KIUCHUMI
|
12,897,721,200.00 |
Jamii |
MASTERCARD FOUNDATION
|
|
Hatimiliki@2017Halmashauri ya Wilaya ya Igunga. Haki zote zimehifadhiwa