Afisa Elimu Taaluma Mkoa Tabora, Bwana Emmanuel Malima, amewakumbusha maafisa elimu msingi, maafisa elimu Kata pamoja na walimu wakuu wa shule za msingi, wilayani Igunga kutunza vishikwambi walivyopewa kwa kuwa ni mali ya Serikali na Mwajili katika ukumbi wa St.Leo mjini Igunga hivi karibuni.
“Kuna mifumo mitatu ya kutolea taarifa ambayo ni mfumo wa taarifa za shule Student Information System (SIS), Mfumo wa Usajili wa taarifa za wanafunzi shule za Msingi ambao ni Basic Education Management Information Systems (BEMIS) na Mfumo wa takwimu za elimu msingi kwa kiingereza Primary Record Manager (PREM)” aliongeza Afisa Elimu Taaluma Mkoa wa Tabora.
Bwana Emmanuel Malima, akiongea na maafisa elimu pamoja na maafisa elimu Kata na walimu wakuu wa shule za msingi wilaya ya Igunga, aliendelea kusisitiza kuwa Katika zoezi la kufatilia vishikwambi na kuhuwisha Mfumo kutoka 2.0.5 kwenda 2.0.6 ambao umeboreshwa, mifumo hii ni muhimu kwa Taifa letu na Elimu ya Tanzania kwani taarifa zilizo sahihi zinatoka katika ngazi ya mwalimu mkuu, ambaye ndiye chanzo sahihi cha kuandikisha mwanafunzi na takwimu zote za msingi zipo kwake.
Aliongeza kuwa vishikwambi hivyo vimetolewa kwa ajili ya kazi ya Takwimu na si kwa ajili ya kuvitumia kwa matumizi yasiyo rasmi, hasa kupigia picha za harusi na kuazimana na kupakua miziki. Aliendelea kuwasisitiza kuwa atakayepoteza kishikwambi utaratibu unajulikana kwa aliyepoteza mali ya Serikali, taarifa zitolewe Polisi kwani amepoteza mali ya Serikali na taarifa muhimu za wanafunzi na walimu hivyo ajiandae kulipa kwa kununua kishikwambi kipya.
Pia aliwataka kusimamia taaluma ipasavyo kwa kuanzisha makaundi ya kujisomea ya wanafunzi watatu watatu ambayo yatapunguza wanafunzi wasiojua kusoma ,kuandika na kuhesabu hasa darasa la tatu na darasa la nne ambao wanaelekea kwenye Mitihani ya Taifa.
Nae Kaimu Afisa Elimu Msingi Bi Martha Bayo, aliwakumbusha maafisa elimu kata hao pamoja na walimu wakuu, kuzingatia maagizo ya Serikali na maelekezo ya pesa zinazopelekwa mashuleni walipe kulingana na vifungu na taratibu, miongozo na Kanununi za Serikali zinavyowaelekeza.
Pia aliwataka kuandaa taarifa mbalimbali zinazohusiana na pesa za Serikali, kwa kuwakumbusha kuwa zinatakiwa kuingizwa kwenye mfumo wa malipo ya fedha uitwao Facility Financing Accounting and Reporting Systems (FFARS) ambao unatakiwa kutumika kuandaa malipo yote ya pesa za Serikali zinazopelekwa mashuleni.
Hatimiliki@2017Halmashauri ya Wilaya ya Igunga. Haki zote zimehifadhiwa