Kaimu Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Igunga ndg, Samwel Hadon Ntulila,amemtuka mkandarasi anayejenga mradi wa maji isenegeja, kuongeza kasi ili aendane na Mkataba katika kikao cha tathimini kilichofanyika Ofisi ya Kata ya Mwisi hivi karibuni.
Kaimu Mkurugenzi amempongeza mkandarasi kuwa ujenzi unaendelea vizuri, hivyo mabomba ambayo yameshatandikwa kwa ajili ya kupitisha maji yaongezwe kwa wakati na Dp tano ambazo hazijakamilika kati ya kumi na tano zilizopo kwenye mkataba zikamilishwe kwa wakati.
“Napenda kumpongeza Mkandarasi kwa kazi nzuri, pamoja na kuwashirikisha wananchi kwa kuibua mradi na kutoa mawazo yakasikilizwa” alisema Kaimu Mkurugenzi. Mradi utakuwa endelevu kwani umetokana na mahitaji yao makubwa ya maji.
Nae Mheshimiwa Diwani Kata ya Mwisi Mhe.Daudi Luziga na Mheshimiwa Stephania Maige Viti maalum Kata ya mwisi waliwataka kamati ya maji kuangalia upya njia sahihi ya wafugaji kupata mabilika ya kunyweshea Mifungo, kwani katika Miradi mingi mifungo haijazingatiwa.
Nae John wangwe Kaimu Mhandisi wa Maji Wilaya ya Igunga, aliwataka Waheshimiwa madiwani na kamati ya maji kuwaelimisha wananchi kutumia maji wakati mradi utakapo kamilika,kwani lengo la serikali ni kuwapatia wananchi maji safi na salama.
Mwakilishi wa mkandarasi Monimar Company Ltd anayejenga mradio huo, wa maji kijiji cha Isenegeja alisema changamoto ya mvua kunyesha katika kipindi cha ujenzi wa tenki, kimesababisha ucheleweshaji wa kumwoga zege na kutandika mabomba. Aliendelea kusema tenki limefika asilimia 50%, na kuwa bomba zimetandikwa kwa kilometa 1.5, ambazo ni sawa na asilimia 89%.
Katibu kamati ya maji na wanakamati waliomba kuongezwa kwa Dp, katika maeneo yenye mkusanyiko wa watu hasa katika Kitongoji C.Pia Kamati ya maji pamoja na Waheshimiwa madiwani walipewa taratibu za kuunganishiwa maji mradi utakapo kamilika.
Hatimiliki@2017Halmashauri ya Wilaya ya Igunga. Haki zote zimehifadhiwa