Mheshimiwa Mkuu wa Wilaya Igunga, Mhe.John Gabriel Mwaipopo amewataka wanawake wa Wilaya ya Igunga kuungana kwa kuanzisha vikundi vya akina mama ili waweze kujikomboa katika shughuli za kiuchumi kuendana na uchumi wa vikwanda hivi karibuni.
Mhe,Mkuu wa Wilaya, aliendelea kuwaelekeza akina mama wote kufanya kazi kwa kujituma, ili kuweza kufikia uchumi wa viwanda kama ilivyo sera ya nchi ili kufikia uchumi wa kati.Aliwataka kuanzisha viwanda vidogo vidogo ambavyo vitawaongezea kipato cha familia pamoja na kukuza mitaji yao na kukuza uchumi wa nchi.
Sambamba la maadhimisho hayo watumishi na wananchi wote walishiriki katika kufanya usafi wa mji wa Igunga ikiwa ni sehemu ya kuufanya mji kuwa msafi na kuwaakumbusha wananchi kuwa na tabia ya kufanya usafi mara kwa mara ili kuweza kuondokana na magonjwa ya mlipuko yanayoweza kujitokeza kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha Wilaya humo.
Nae Kaimu Mkuu wa Idara ya usafi na Mazingira Bwana Fredrick Mnahela, aliwaasa wananchi kujitokeza kila siku ya alhamisi kufanya usafi katika makazi yao ili kuweka mji safi. Pia aliwataka wananchi kutotupa uchafu kwenye mitaro kwani inasababisha kuziba na maji kushindwa kutembee na kuharibu barabara. Hivyo kuwaasa kuanza kulipia tozo za taka kwa mawakala watakao kuwa wanapita na kuzoa taka hizo.
Na,Apollo P.Daudi Igunga DC
Hatimiliki@2017Halmashauri ya Wilaya ya Igunga. Haki zote zimehifadhiwa