MKUU wa Wilaya ya Igunga mkoani Tabora, Mhe. Sauda Mtondoo amesema wanasimama kifua mbele kwa kutekeleza Ilani ya Chama cha Mapinduzi (CCM) kutokana na ushirikiano ambao Baraza la Madiwani walimpatia.
Mhe. DC. Sauda ametoa kaluli hiyo Jumatano Mei 14, 2025 wakati wa Kikoa cha Baraza la Madiwani lililofanyika katika ukumbi wa Mikutano wa Halmashauri hiyo mjini hapa.
Alisema wametekeleza ipasavyo Ilani hiyo kwa sababu ya kuwepo wa Madiwani katika ngazi ya kata ambako kila fedha iliyolelekezwa katika maeneo yao waliisimamia vema.
‘’Kila mmoja anacho cha kwenda kusema serikali imefanya hivi na mimi nimesimamia hivi, hivyo tusimame kifua mbele kuyaeleza yele mazuri yote tuliyofanya kwa lengo la kuhakikisha wananchi wanaendelea kutupa imani,’’ alisema.
Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo, Lucas Bugota alimshukuru Rais Dk. Smaia Suluhu Hassan kwa kuwateulia viongozi ambao wameendelea kuwa wasikivu na kufanikiwa kuleta maendelo ya Halmashauri.
Alisema wao watapambana kurudi na kuhakikisha kura za Rais Dk. Samia zinapatikana za kishindo huku akiwaomba wateule wake wamuhakikishie kuwa kura zote za Igunga ni zakwake.
Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo, Bi. Selwa Hamid aliwashukuru Madiwani kwa namna ambavyo wamewaongoza na kuahidi kuyatekeleza yote waliyoyaagiza kwa sababu yeye ni muumini wa kutenda haki.
Mbali na shukrani hizo, Bi. Selwa alisema shukran za pekee zimuendee Mhe. Rais Dk. Samia ambae katika awamu ya uongozi wake alielekeza Igunga fedha za miradi ya maendeleo zaidi ya sh. 41.4 bilioni.
‘’Hakika tunakiri miradi mingi tumeitekeleza na inatoa huduma kupunguza adha na changamoto kwa wananchi wetu katika kata 35,’’ alisema.
Katika hatua nyinge, Selwa aliwapongeza Madiwani na Wataalamu kwa kufanikisha Halmashauri hiyo kupata Hati Safi katika mwaka 2020 hadi 2021, 2021 hadi 2022 na 2022 hadi 2023 huku akidokeza huenda na mwaka 2023 hadi 2024 watapata Hati Safi.
Pia, alisema Halmashauri imepiga hatua katika ukusanyaji wa mapato ya ndani kwa kukusanya sh. 4.8 sawa na asilimia 90.27 ambapo ilikua imekusudia kukusanya sh. 5.393 bilioni kwa mwaka wa fedha 2024 hadi 2025.
==== //// ==== //// =====
Hatimiliki@2017Halmashauri ya Wilaya ya Igunga. Haki zote zimehifadhiwa