Mkuu wa Wilaya ya Igunga Mhe; Sauda Mtondoo ametoa maelekezo kwa watendaji wa Kata na watendaji wa Vijiji katika masuala mbalimbali katika Maeneo yao ya Utawala. Katika Kikao kilichofanyika kwenye ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Igunga 29/11/2023,Mhe; Mtondoo amewataka watendaji wa Serikali kwa ujumla wao ndani ya Wilaya kila mmoja atekereze majikumu yake kwa weledi mkubwa. Pia Mkuu wa Wilaya amewataka watendaji wa Kata na Wavijiji kuongeza nguvu katika mapambano dhidi ya Malaria. Mkoa wa Tabora unaongoza kwa maambukizi toka 11.7% 2017/2018 hadi kufikia 23.4% 2023. Wakati kiwango cha maambukizi Kitaifa ni 8.1% Wananchi wasisitizwe matumizi bora ya vyandarua, kutoa Elimu kwa Jamii, kusimamia Usafi wa mazingira kwa wananchi, Kuwashirikisha viongozi wa dini na siasa katika mapambano dhidi ya Malaria.
Kuimarisha kampeni ya usafi wa mazingira ikiwa ni pamoja na ujenzi wa vyoo bora na matumizi ya vyoo hivyo. Sheria ndogo za usafi wa mazingira zitumike, Agizo la ujenzi wa vyoo bora kwa kila Kaya. (Muda miezi 2) baada ya hapo sheria zichukue mkondo wake.
Kuhusu suala la Elimu Mhe Mkuu wa Wilaya ametoa maagizo kwa Watendaji wa Kata na Watendaji wa Vijiji kwenda kusimamia uandikishaji wa watoto wa Elimu ya Awali na Darasa la kwanza kwa mwaka 2024. Hadi tarehe 24/11/ 2023 uandikishaji Elimu ya Awali ulikuwa awali 22% na Darasa la kwanza 40%.
Mdondoko wa wanafunzi: Kimkoa ni asilimia 34.5% ambacho ni kiwango kikubwa, hivyo ni jukumu la kila Mtendaji kufuatilia watoto wote wamalize masomo yao, washule za msingi wamalize Darasa la 7 na wasekondari walioanza Kidado cha kwanza wote wafike kidato cha nne.
Kwenye suala la Kilimo Amewaagiza Watendaji:
Misitu na mazingira Wataalamu wametakiwa Kusimamia zoezi la upandaji miti kwa kila Kaya na maeneo ya Taasisi. Aidha amesisitiza kampeni ya “NASOMA NA MTI WANGU” itiliwe mkazo katika Shule zote za Msingi na Sekondari.
Ukusanyaji wa mapato, Kwa wale wote mwenye POS, wahakikishe wanaweka fedha zote Bank zilizokusanywa.
Marufuku kutumia pesa ya makusanyo ya Serikali kabla ya kuipeleka Benk. (Alisema Mhe; Sauda Mtondoo Mkuu wa Wilaya ya Igunga)
Hatimiliki@2017Halmashauri ya Wilaya ya Igunga. Haki zote zimehifadhiwa