• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Baruapepe |
Igunga District Council
Igunga District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Igunga

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Msingi Mkuu
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Halmashauri
    • Idara
      • Maendeleo ya Jamii
      • Afya
      • Idara ya Elimu Msingi
      • Idara ya Elimu Sekondari
      • Utumishi na Utawala
      • Mazingira
      • Maji
      • Ujenzi
      • Kilimo,Umwagiliaji na Ushirika
      • Maliasili, Ardhi na Mazingira
      • Uvuvi na Mifugo
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Fedha na Biashara
    • Vitengo
      • Teknolojia ya Habari na Mawasiliano
      • Uchaguzi
      • Ukaguzi wa ndani
      • Sheria
      • Ugavi
    • Kata
      • Our Wards
  • Vivutio vya Uwekezaji
    • Vivutio Vya Kitalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Uvuvi
  • Wah. Madiwani
    • Orodha Ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha, Uongozi na Utawala
      • Mipangomiji na Mazingira
      • Kamati ya Uchumi, Elimu na Afya
      • UKIMWI
      • Kamati Ya Maadili
    • Ratiba
      • Vikao Vya Madiwani
      • Meeting With Chairperson
  • Miradi
    • Miradi Itakayo Tekelezwa
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Huduma kwa Mteja
    • Mpango Mkatati
    • Ripoti
    • Fomu
    • Taratibu
  • Vituo vya Habari
    • Press Release
    • Video za Shughuli za Ofisi Kitaifa
    • Makitaba ya Picha
    • Hotuba za Viongozi

KITANZI KITAWAHUSU WAWEZESHAJI WATAKAO KIUKA TARATIBU ZA UTAMBUZI KAYA MASKINI

Tarehe iliyowekwa: July 7th, 2021

Mhe. Sauda Salum Mtondoo ambae ni Mkuu wa Wilaya ya Igunga amewataka  wawezeshaji,waheshimiwa madiwani pamoja na viongozi wote kuwa, Serikali iliagiza kutolewa elimu ya kutosha na kujenga uelewa wa pamoja kwa jamii ili kuondoa malalamiko kwa jamii,amesema jana katika kikao kazi kilichofanyika katika ukumbi wa halmashauri ya Wilaya ya Igunga

Serikali iliagiza wawezeshaji na viongozi watakao shiriki katika zoezi hili la kutambua walengwa na kuandikisha wawe walengwa wanaostahili, aliwataka kuzingatia vigezo vilivyowekwa ili kupata walengwa sahihi

“Kupitia viapo mtakavyo apa  vitawaweka kwenye kitanzi,iwapo mtakiuka taratibu za utambuzi wa kaya masikini, atakae ingia kwenye mpango huu awe ni yule mwenye vigezo na vizingatiwe kusiwe na undugu wala upendeleo katika uandikishaji”alisisitiza Mhe.Mkuu wa Wilaya Igunga

Aidha aliwataka wawezeshaji watakao onekana wamekiuka taratibu katika zoezi hili la uandikishaji, wasimamizi wa zoezi hili kuwachukulia hatua stahiki

 “Mapambano dhidi ya umasikini katika nchi yetu yalianza toka baada ya Uhuru takribani miaka sitini  sasa na bado tunaendelea kupambana nayo utekelezaji wa shughuli za TASAF ni moja ya nyezo za kupambana na umaskini, kaya zaidi ya milioni moja zimewezeshwa na TASAF kupambana na umasikini” ameyasema hayo katika Kikao kazi  Sauda Salumu Mtondoo Mhe.Mkuu wa Wilaya Igunga

Pia wale ambao hali zao za kiuchumi hazijaimalika hawataachwa bali wataendelea kupatiwa elimu ili kuondokana na umaskini, ili kuendelea kuboresha kaya zao aliongeza Mhe. Sauda Salum Mtondoo, Mkuu wa Wilaya Igunga

Amewataka viongozi walioshiriki kikao kazi hicho kuwa  wanajukumu la kuendelea kuwapa msaada walengwa kwa kuendelea kuwakwamua kiuchumi kwa kuhakikisha watumishi wanaofatilia shughuli za walengwa kujiimalisha katika sekta za mifugo,kilimo na ujasiliamali ili waweze kuwaelimsha kuboresha uchumi wao

Akiongea Mwakilishi wa Mkurugenzi Mtendaji TASAF Makao Makuu Bwana Oscar Maduhu alisema kutokana na malalamiko kutoka kwenye jamii kuwa ndani ya walengwa kuna walengwa hawana vigezo au  walengwa hewa ili kuwaondoa kwenye mpango hasa kaya zisizokuwa na vigezo, za viongozi, waliohama na waliofaliki zoezi hili lilifanyika katika kipindi cha mwezi wa sita 2020 na kurudiwa Disemba 2020, lengo lake lilikuwa ni kusafisha au kuhuisha daftari la walengwa au masjala ya walengwa iliyopo TASAF Makao Makuu

Kipindi cha pili cha awamu ya tatu ya mfuko wa Maendeleo ya Jamii TASAF kitatekelezwa katika halmashauri zote 184 za Tanzania bara na  wilaya zote za Zanzibar kitafikia kaya 1,450,000 zenye jumla ya watu zaidi ya milioni 7,000,000 kote nchini

Mkazo mkubwa katika kipindi cha pili cha awamu ya tatu ya TASAF umewekwa katika kuwezesha kaya zitakazo andikishwa kwenye  kufanya kazi na  kuongeza  ili kuongeza kipato,  aidha kipindi cha pili cha awamu ya tatu ya mfuko wa Maendeleo ya Jamii TASAF kitahakikisha huduma za jamii  zinaongezwa na kuboreshwa na kutoa huduma na kuendeleza rasilimali watoto hususani katika upatikanaji wa elimu na afya

Bwana Oscar Maduhu ameendelea kusema walengwa watatambuliwa na kuandikishwa kipindi cha pili cha awamu ya tatu ya mfuko wa Maendeleo ya Jamii TASAF, ni kaya zinazoishi katika hali duni katika vijiji, mitaa na shehia zetu.

Wanufaika ndani ya kaya ni  watoto chini ya miaka 5 wanaohudhuria kliniki, wanafunzi shule za awali,shule za msingi na shule za sekondari,mama wajawazito na wana kaya wenye ulemavu ameongeza Bwana Oscar Maduhu

Aidha ameendelea kusema mpango unatoa ruzuku za aina mbili ruzuku ya  msingi na ruzuku ya masharti kwa wale wanaotakiwa kwenda shule na watoto wanaohudhuria kliniki, lakini ajira za muda kwa mwanakaya mmoja aliye na uwezo wa kufanya kazi

Aliendelea kumshukuru Mkurugenzi mtendaji Wilaya kwa kutoa wataalam wengi kutoka ngazi ya kata kushiriki katika zoezi la kutambua na kuandikisha walengwa, aidha watasaini  viapo vya uadilifu ambavyo vitatumika pale ambapo mwezeshaji ataandikisha kaya ambazo hazina vigezo viapo hivyo vitatumika pia kwa viongozi wa mitaa na vijiji

Amewaomba viongozi kutoa ushirikiano wataokuwepo kwenye maeneo zoezi litakapo kwenda kufanyika taarifa zitolewe mapema na viongozi watende haki na kuepuka  upendeleo katika uandikishaji walengwa ili wale wanaostahili     waweze kuandikishwa.

Matangazo

  • TANGAZO LA KUKODISHA SHAMBA LA BULYASHIRI LINALOMILIKIWA NA H/W IGUNGA October 03, 2022
  • TANGAZO LA KUITWA KAZINI IGUNGA DC September 05, 2022
  • TANGAZO LA NAFASI YA KAZI MAALUMU YA KUKUSANYA USHURU HALMASHAURI YA WILAYA YA IGUNGA August 24, 2021
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI November 24, 2020
  • View All

Habari Mpya

  • JOGGING PAMOJA NA MAZOEZI

    March 05, 2023
  • BARAZA LA MADIWANI LAPITISHA BAJETI YA MWAKA 2023/2024

    March 05, 2023
  • Mh.Mkuu wa Wilaya Igunga Akabidhi Pikipiki Saba kwa Watendaji wa Kata Wilayani Igunga

    March 01, 2023
  • ZIARA YA KATIBU UENEZI CCM TAIFA WILAYA YA IGUNGA

    September 13, 2022
  • View All

Video

Maadhimisho ya siku Wanawake Kata Simbo ya SIMBO wilayani Igunga.
Video Zaidi

Viungio vya haraka

  • Hotuba
  • Pakua Fomu
  • Zabuni
  • Matangazo ya kibiashara
  • Matukio

Kurasa zinazofanana

  • Watumishi Portal
  • Poralg
  • Public Service Management
  • Tabora Region Website
  • NECTA

World visitors tracker

world map hits counter

Waliotembelea

writingMasterThesis

Ramani

Wasiliana nasi

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya mara kwa mara
    • Sitemap
    • Huduma
    • Huduma

Hatimiliki@2017Halmashauri ya Wilaya ya Igunga. Haki zote zimehifadhiwa