Asilimia 97 ya wakazi wa wilaya ya Igunga wanategemea sana kilimo kama shughuli kuu ya kiuchumi na kujiongezea usalama wa chakula.
Wilaya ya Igunga inazalisha mazao ya chakula na biashara. Mazao ya chakula ni mahindi, mpunga, muhogo, viazi vitamu, mtama na mikunde. Mazao ya biashara ni pamba, alizeti, karanga,ufuta, choroko na korosho
Wilaya ya Igunga inazalisha mazao mengine ya biashara ukiacha zao la mpunga na pamba ambayo yanaweza kufanyiwa uwekezaji wa kibiashara na yakaleta tija kwa maendeleo ya wakulima na wilaya kwa ujumla wake. Mazao hayo ni alizeti, choroko na ufuta
Jedwali: Uzalishaji wa mazao haya kwa misimu 2014/2015 hadi 2017/2018
MSIMU |
Mazao |
||
Alizeti (tani) |
Choroko (tani) |
Ufuta (tani) |
|
2014/ 2015 |
2,548 |
11,199 |
2,024 |
2015/ 2016 |
4,976 |
13,502 |
1,480 |
2016/ 2017 |
2,104 |
2,934 |
1,989 |
2017/2018 |
6,080 |
2,792 |
2,512 |
Fursa za kibiashara zinazotokana na mazao ya alizeti, choroko na ufuta
Vivutio vya kibiashara
Fursa za kibiashara katika zao la pamba
Wilaya ya Igunga ndiyo inaongoza kwa uzalishaji wa pamba katika mkoa wa Tabora. Asilimia 94 ya pamba yote inayozalishwa mkoani Tabora inatoka wilaya ya Igunga. Eneno linalolimwa pamba hapa wilayani limekuwa likiongezeka kila mwaka ingawaje mavuno yake yamekuwa yakiathiriwa na hali ya ukame na mlipuko wa wadudu/ magojwa ya mimea.
Uzalishaji wa pamba wilayani igunga misimu ya 2014/2015 hadi 2017/2018
Jedwali : Uzalishaji wa zao la pamba msimu 2013/14 hadi 2017/2018
MSIMU |
LENGO (Ha) |
UTEKELEZAJI (Ha) |
UZALISHAJI (Tani) |
2013/2014
|
24,020
|
22,550
|
17,700
|
2014/2015
|
24,020
|
21,112
|
16,100
|
2015/2016
|
24,020
|
22,180
|
10,900
|
2016/2017
|
24,020
|
18,440
|
10,700
|
2017/2018
|
33,330
|
56,608
|
16,400
|
Kielelezo: Uzalishaji wa zao la pamba ukilinganisha na malengo, utekelzaji na uzalishaji
Kutokana na uwezo wa kuzalisha pamba kwa kiasi kikubwa, fursa za kibiashara katika sekta ndogo ya pamba ni kama ifuatavyo:-
Vivutio katika kibiashara
Fursa za kibiashara katika kilimo cha umwagiliaji
Halmashauri ya wilaya ya igunga ina eneo la jumla ya hekta 11,547 zinazofaa kwa kilimo cha Umwagiliaji. Maeneo ambayo yamebainishwa kwa ajili ya uwekezaji wa kibiashara wa kilimo cha Umwagiliaji kwa uzalishaji wa zao la mpunga ambalo ndiyo zao la kipaumbele linalofaa kwa chakula na biashara hapa wilayani yana eneo la hekta 8,097. Mchanganuo wa maeneo yanayofaa kwa uwekezaji wa kibiashara wa kuzalisha zao la mpunga kwa njia ya umwagiliaji ni kama ifuatavyo:-
Jedwali: Maeneo yanayofaa kwa kibiashara wa kilimo cha umwagiliaji wilayani Igunga
Na
|
Kata
|
Kijiji
|
Zao linalofaa kuzalishwa
|
Eneo linalo hitaji kibiashara (ha)
|
Eneo lenye miundo mbinu (ha)
|
1
|
Igunga
|
Mwanzugi
|
Mpunga |
1,500 |
630 |
2
|
Igoweko
|
Buhekela
|
Mpunga |
750 |
400 |
3
|
Igurubi
|
Igurubi
|
Mpunga |
600 |
400 |
4
|
Choma
|
Choma
|
Mpunga |
400 |
320 |
5
|
Mbutu
|
Mbutu
|
Mpunga |
350 |
0 |
6
|
Isakamaliwa
|
Isakamaliwa
|
Mpunga |
380 |
0 |
7
|
Simbo
|
Simbo
|
Mpunga |
2,500 |
0 |
8
|
Kinungu
|
Mwamapuli
|
Mpunga |
400 |
400 |
9
|
Igunga
|
Makomero
|
Mpunga |
617 |
0 |
10
|
Mwashiku
|
Mwashiku
|
Mpunga |
400 |
0 |
11
|
Itumba
|
Itumba
|
Mpunga |
200 |
157 |
|
JUMLA
|
|
|
8,097 |
2,307 |
Aina ya fursa za kibiashara unaohitajika katika eneo hili la kilimo
Maeneo makubwa yanayofaa kwa kilimo cha Umwagilaji
Ujenzi wa mabwawa makubwa
Miundombinu ya Umwagiliaji
Vivutio vya kibiashara katika kilimo cha umwagiliaji wa zao la mpunga
Hatimiliki@2017Halmashauri ya Wilaya ya Igunga. Haki zote zimehifadhiwa