JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
OFISI YA RAIS TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA HALMASHAURI YA WILAYA YA IGUNGA |
Simu: +255 (026) 2650019 (G/L) Halmashauri ya Wilaya,
+255 (026) 2650021 (D/L) 16 Mtaa wa Bomani,
Nukushi: +255 (026) 2650242 45682 Igunga Urban.
Barua pepe:ded@igungadc.go.tz S.L.P. 19,
Tovuti: http://www.igungadc.go.tz IGUNGA – TABORA
Unapojibu Tafadhali taja:-
Kumb. Na. AB.285/294/01/64 16 Julai, 2024
TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI
Mkurugenzi amepata kibali kipya cha ajira kwa ikama ya mwaka 2023/2024 chenye Kumb. Na. FA. 97/288/01/09 cha tarehe 25.06.2024 kutoka kwa Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora. Kufuatia kibali hicho Mkurugenzi wa Halmashauri ya Igunga anakaribisha maombi kwa watanzania wenye sifa za kujaza nafasi za kazi zifuatazo :-
Kuajiriwa mwenye elimu ya kidato cha nne/sita aliyehitimu mafunzo ya Astashahada/Cheti (NTA LEVEL 5) katika mojawapo ya fani zifuatazo: Utawala, Sheria, Elimu ya Jamii, Usimamizi wa Fedha, Maendeleo ya Jamii na Sayansi ya jamii kutoka chuo cha Serikali za Mitaa au chuo chochote kinachotambuliwa na Serikali.
Kwa kuzingatia ngazi za mishahara ya Serikali – TGS B.
Awe na Elimu ya kidato cha Nne (Form IV) au cha Sita (Form VI) aliyehitimu mafunzo ya Stashahada/Diploma (NTA Level 6) katika fani ya masjala kutoka katika vyuo vinavyotambuliwa na Serikali, wenye ujuzi wa compyuta.
Kwa kuzingatia ngazi za mishahara ya Serikali – TGS C
Awe amehitimu kidato cha nne (IV) na kupata Cheti cha Mtihani wa Kidato cha Nne (IV). Awe na leseni daraja ‘C’ au “E” ya uendeshaji pamoja na uzoefu wa kuendesha magari kwa muda usiopungua mwaka mmoja (1) bila kusababisha ajali, Awe amehudhuria mafunzo ya msingi ya Uendeshaji Magari (Basic Driving Course) yanayotolewa na chuo cha Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) au Chuo kingine kinachotambuliwa na Serikali.
Kwa kuzingatia Ngazi ya Mshahara ni TGS B
MUHIMU: Kumbuka kuambatisha barua yako ya maombi ya kazi iliyosainiwa pamoja na vyeti vya elimu, Anuani ya barua hiyo ielekezwe kwa;
Maombi yote yatumwe kwenye mfumo wa kielectroniki wa Ajira (Recruitment Portal) kupitia anuani ifuatayo; https://portal.ajira.go.tz// (Anuani hii pia inapatikana kwenye tovuti ya Sekretarieti ya Ajira kwa kuingia sehemu iliyoandikwa ‘Recruitment Portal’)
Limetolewa na:-
Hatimiliki@2017Halmashauri ya Wilaya ya Igunga. Haki zote zimehifadhiwa